June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

OSHA yaongeza ukusanyaji takwimu za viwanda

Spread the love

MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) imeongeza kukusanya takwimu za usajili wa viwanda na sehemu za kufanyia kazi kutoka 60 kwa wiki na kufikia 150. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu OSHA, Dk. Akwilina Kayumba amesema, takwimu hizo zilianza kuchukuliwa baada ya agizo la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Jenista Mhagama alilolitoa Desemba 14 mwaka jana kupitia vyombo vya habari.

Katika agizo lake hilo Mhagama aliwataka wamiliki wote wa sehemu za kazi na wakala kusajili ndani ya siku 14 ambapo lilianza kutumika tangu Desemba 14 mwaka jana.

Aidha, Kayumba amesema, kwa mujibu wa kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Usalama na Afya ya mwaka 2003 kinamtaka mmiliki yeyote wa kiwanda au sehemu ya kazi kusajiliwa na wakala kabla ya kuanza na shughuli za uzalishaji katika sehemu husika.

“Kimsingi kusajili sehemu za kazi kunamuwezesha Mkaguzi Mkuu (AG) ambaye ndiye mtendaji mkuu wa wakala ili kuzitambua sehemu zote za kazi na hivyo kuweza kupanga utaratibu wa kuzitembelea na kufanya ukaguzi ili kujiridhisha kama masuala yote yanayohusu usalama na afya mahali pa kazi yanazingatiwa na hatimaye kutoa leseni za kazi,” amesema Kayumba.

Ameeleza kuwa, pamoja na kwamba wamiliki wengi wamejitokeza na kuitikia wito wa waziri na kuongeza idadi ya takwimu, lakini bado inaonesha kuna idadi kubwa ya sehemu za kazi ambazo bado hazijasajiliwa.

“Tunawataka wamiliki ambao hawajatekeleza agizo la Waziri wahakikishe wanatekeleza mara moja kabla hawajafikiwa na oparesheni yetu ya kuwatambua inayoendelea nchi nzima,” amesema Kayumba.

error: Content is protected !!