July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Osha wawezesha akinamama Dodoma

Spread the love

WAKALA wa usalama mahala pa kazi nchini (Osha) wametoa mafunzo kwa akinamama zaidi ya 60 wa Manispaa ya Dodoma wanaofanya kazi katika vumbi la nafaka pamoja na kuwapatia vifaa vya kuwakinga na madhara mbalimbali yatokanayo na kazi hiyo, Anaandika Dany Tibason.

Akizungumza katika mafunzo hayo Akwilina Kayumba Mtendaji mkuu wa wakala wa usalama mahala pakazi, alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia akinamama hao kujikinga na madhara mbalimbali yataokanayo na kazi hiyo.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wajasilimali mbalimbali nchini namna ya kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na kazi wanazozifanya lakini kundi hilo walikuwa bado hawajalifikia.

“Tulikuwepo hapa Dodoma kipindi cha nyuma na tulitoa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 50 lakini hawa ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kupembua nafaka ambazo zinakuwa kwenye mavumbi kama vile ufuta na nyinginezo lakini hatukuwa tumewapatia mafunzo yoyote na hii leo wameweza kupata fursa ya mafunzo haya pamoja na vifaa vya kuwakinga”alisema Kayumba.

Aliongeza kuwa katika vumbi la nafaka ambazo akina mama hao wamekuwa wakipembua mazao ya aina mbalimbali pamekuwepo na vumbi ambalo ni hatari kwa afya zao kwakuwa linaweza kusababisha kupata kansa ya ini.

“Katika vumbi la kalanga kuna fangasi ambao wanaweza kusababisha kansa ya ini ambayo sumu hiyo inaitwa (aflatoxin) ambayo kwa Kiswahili inafahamika kama sumukuvu ambayo ni hatari kwa afya za akinamama hao”alisema Kayumba.

Alisema kuwa pamoja na kansa ya Ini pia vumbi ambalo wamekuwa wakilipata kila wanapofanya kazi hiyo linasababisha pia madhara mbalimbali ikiwemo kifua.

Kayumba alisema kuwa pamoja na kuwapatia mafunzo hayo ya namna ya kujikinga pia wamewapatia vifaa kama vile maski ambazo watakuwa wanazitumia wakati wa kupembua vumbi lililopo katika nafaka mbalimbali.

Mmoja wa akinamama hao waliopatia mafunzo Merina Daudi, alisema kuwa wanaishukuru Osha kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuzilinda afya zao.

Alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya elimu kwa akinamama hao ambao wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira hatarishi kiasi mabacho kinawasababisha madhara makubwa katika afya zao.

“Tunawashukuru sana Osha kwa mafunzo haya pamoja na kutupatia vifaa ambavyo tutavitumia katika kujirinda na afya zetu kwani hapo awali hatukuwa navyo”alisema Daudi.

error: Content is protected !!