October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

OSHA kuwafikia wajasiriamali katika mazingira hatarishi

Watengeneza batiki

Spread the love

WAKALA wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) umesema uko katika mkakati wa kuwafikia wajasiriamali, wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 2 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam, Hadija Mwenda, Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA, amesema wajasiriamali wengi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi, kutokana na kutofikiwa na wakala huo.

Mwenda amesema OSHA ilishindwa kuwafikia wajasiriamali hao, kwa sababu ya kutosajiliwa, hali iliyosababishwa na kutokuwa na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao.

Kufuatia changamoto hiyo, Mwenda amesema OSHA imeanza utaratibu wa kuwafikia wajasiriamali hao, kwa lengo la kuwashauri namna ya kujikinga na mazingira hatarishi, kwenye mahala pa kazi.

Mwenda amesema hadi sasa OSHA imewafikia wajasiriamali 28,000 nchi nzima, na kwamba utaratibu huo ni endelevu ili kuhakikisha kundi hilo linafikiwa.

“Tuko kwenye mkakati wa namna ya kuwafikia wajasiriamali, sababu wanafanyakazi katika mazingira magumu na hatari. Mfano watengenezaji wa batiki hutumia kemikali hatari pasipo kuwa na elimu juu ya madhara yake na namna ya kujikinga,

Vvile vile mafundi gereji nao wako katika mazingira hatarishi. Hii yote ni kwa sababu hawajasiliwa. Inakuwa changamoto kuwajua walipo na namna ya kuwafikia,” amesema Mwenda.

error: Content is protected !!