May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Oscar Oscar ajitosa kumdhibiti Karia TFF

Oscar Oscar

Spread the love

 

MCHAMBUZI wa soka kutoka kituo cha radio cha E-FM, Oscar Oscar amejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 7 Agosti, 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Uchaguzi huo ambao kwa mwaka huu utafanyika mkoani Tanga ambapo mpaka sasa waliojitokeza kuchukua fomu kwenye nafasi ya Urais ni wawili.

Mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Oscar Oscar, alisema kuwa lengo lake ni kuongoza mpira wa Afrika na Dunia, lakini kwa sasa lazima aanzie nyumbani.

“TFF kwangu kama mwanzo tu, lengo langu kuu ni kuongoza mpira wa Dunia na hisani uanzia nyumbani, hauwezi kwenda kuubadilisha mpira wa Afrika au Dunia, bila kuubadilisha mpira wa nyumbani ndiyo maana nikaamua kuja kuchukua fomu,” alisema Oscar Oscar.

Katika hatua nyingine Oscar, alisema katika kazi yake ya uchambuzi kwenye radio, alikuwa akitoa maoni, lakini sasa anataka kuingia kwenye vyombo vya maamuzi.

Oscar Oscar anakuwa mtu wa pili kuchukua fomu kwenye nafasi hiyo mara baada ya Wallace Karia, kuchukuliwa fomu jana na wadau wa mchezo wa mpira baada ya kumaliza kipindi chake cha awali cha uongozi.

Zoezi hilo la uchukuaji fomu lilifunguliwa jana tarehe 8 Juni, 2021, na litafungwa tarehe 12 Juni 2021, majira ya saa 1o jioni.

error: Content is protected !!