October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Orodha majaji wala rushwa yamfikia JPM

Rais John Magufuli akiteta jambo na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma

Spread the love

ORODHA ya majina ya baadhi ya majaji wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya rushwa imemfikia Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Novemba 2018, Rais Magufuli amesema wapo majaji wanachukua rushwa, na kwamba ana majina ya majaji takribani wanne wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo.

Rais Magufuli amesema baadaye atayafikisha majina hayo kwa Jaji Mkuu Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

“Wapo majaji wanachukua rushwa, baadae jaji mkuu nitakuletea majina,majaji wapo kama wanne,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!