January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Operesheni ‘Okoa Tembo Tanzania’ yazinduliwa Dar

Spread the love

WANAHARAKATI wa Okoa Tembo wa Tanzania wameitaka serikali kuwakamata na kuwashitaki wafanyabiashara wakubwa wa biashara ya meno ya tembo nchini ili kuokua maisha ya viumbe hao wanaonekana kupungua kwa kasi nchini. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yamezungumwa na wanaharakati hao walipokutana na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ili kuzindua kampeni yao ya “Okoa Tembo Tanzania.”

Wanaharakati hao wamesema kuwa idadi ya tembo nchini Tanzania imezidi kupungua kutoa tembo 109,000 mwaka 2009 hadi tembo 43,000 kwa mwaka 2014, ambapo wameitaka serikali kuchukua juhudi za makussudi ili kuhakikisha wanyama hao wanalindwa ipasavyo.

Shuberti Mwarabu, kiongozi wa kampeni hiyo, amesema kuwa serikali ya Tanzania ifanye ushawishi kukomeshwa kwa biashara hii katika nchi ya China ambayo ndio soko kubwa la meno ya tembo duniani ambapo wanaifanya biashara hiyo kama biashara ya kawaida.

“Kule china meno ya tembo ni biashara halali ambapo kuna soko maalum la uuazaji na ununuaji wa meno ya tembo ambapo inasadikika asilimia 90 ya men ohayo yanatoka Tanzania,” amesema Mwarabu.

Lameck Mkuburo, ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo, ameitaka serikali kuwakamata na kuwashitaki wafanya biashara wakubwa wa biashara hiyo bila kujali hadhi, utaifa, na mamlaka yao, kwani, kwa kufanya hivyo tutaweza kuvunja mtandao wa majangili hao.

Arafat Mtui, mjumbe wa kampeni hiyo, amedai kuwa kampeni hiyo ni endelevu na kwamba ameitaka serikali ya awamu ya tano kuteketeza hadharani ghala kuu iliyohifadhi meno ya tembo ili kuonyesha kuwa ni mwisho wa thamani ya meno ya tembo na Tanzania itakuwa nchi ambayo inathamini kiumbe huyo.

“Tungependa kuona ile ghala iliyokuwepo pale wizara ya maliasili inateketezwa kwa moto hadharani ili kuonyesha kuwa biashara hiyo imefikia mwisho,” amesema Mtui.

Wadau wengine wanaosaidia kampeni hiyo ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Sokoine, Professa Kidengesho , Mhifadhi wa Idara ya Wanyama Pori Benson Kibonde, Mwanahabari Charles Hilal na Milladi Ayo.

Wanamuziki pia ni mabalozi wa Wanyama pori. Wanawakilishwa na Vanessa Mdee. Vyombo vya habari kama vile gazeti la the Guardian, gazeti la Mwanachi, televisheni ya ITV na redio ya Radio One navyo havijabaki nyuma.

error: Content is protected !!