September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Operesheni Dar yakamata SMG mbili

Spread the love

JESHI la Polisi limefanikiwa kukamata silaha mbili aina ya SMG zilizokuwa zimefichwa maeneo ya Yombo Relini, jijini Dar es Salaam, anaandika Aisha Amran.

Silaha hizo zimepatikana baada ya oparesheni endelevu inayofanyika jijini humo ya kukamata wahalifu wa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Aidha wakati wa msako huo askali walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, Shaban Ramadhani (35), Mkazi wa Mbande ambaye anadaiwa kujihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Simon Sirro, Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema, mtuhumiwa huyo baada ya mahojiano, aliwapeleka askali katika chumba cha mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Fatuma Salehe (20) ambaye ana uhusiano naye wa kimapenzi na baada ya kupekuwa katika chumba hicho, ndipo ilipatikana silaha hiyo ikiwa imekatwa kitako pamoja na risasi 10 ndani ya magazine.

Amesema, upekuzi pia ulifanyika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo maeneo ya Mbagala, Mbande na Kisewe ambako walifanikiwa kupata bunduki yenye namba UB-9686-1998 ikiwa na magazine tupu.

Sirro amesema, upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa siraha hizo na upelelezi utakapokamilika kuhusu mtuhumiwa huyo kushiriki kwake kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha atafikishwa vmahakamani kwa hatua zaidi.

Katika oparesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 482 wamekamatwa mpaka sasa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na Bhangi, kete,puli na gongo, kosa la kubuguzi abiria pomoja na kosa la kujihusisha na vitendo vya unyang’anyi wa kutumia silaha.

error: Content is protected !!