Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ongezeko migogoro ya wafugaji: Serikali yashauriwa kufumua Sheria, sera
Habari Mchanganyiko

Ongezeko migogoro ya wafugaji: Serikali yashauriwa kufumua Sheria, sera

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa
Spread the love

 

KUFUATIA ongezeko la migogoro ya wafugaji nchini, Serikali imeshauriwa kufumua Sheria na sera zinazosimamia sekta ya mifugo, ili ziendane na wakati kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa jana Jumanne, na Mchambuzi wa masuala ya ufugaji, Onesmo Olengurumwa, akichambua hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyoitoa katika mkutano wa wadau wa sekta ya mifugo, uliofanyika tarehe 19 hadi 20, Desemba 2022.

Olengurumwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa THRDC ameeeleza kuwa, ili kuwe na mabadikiko na maboresho ya kudumu yenye tija na faida Kwa sekta ya mifugo na wafugaji, lazima Sheria na Sera ya Mifugo, ziboreshwe.

“Waziri mkuu ameeleza kuwa, Serikali imekuwa ikipitisha sheria, sera na mipango mbalimbali katika sekta hii ikiwemo suala la ongezeko la bajeti ya mifugo. Hili eneo binafsi bado naliona pengine kuna changamoto kwenye namna tunavyoshirikisha wafugaji katika kufanya maboresho ya Sheria. Tunayo matatizo mengi ya kisera na kisheria ambayo ili kuweza kuwa na mwelekeo mzuri wa sekta ya mifugo ni lazima turudi kupitia upya sera na sheria zetu,”

” Tuwe na sera inayotambua mfumo wa ufugaji asili ulioboreshwa. Bahati nzuri nilishawahi chambua sera ya mifugo Tanzania, sera hii haitambui kabisa ufugaji asili, zaidi imeegemea kwenye ufugaji wa kisasa bila kuwa na mwelekeo mzuri wa ufugaji wa asili,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa ametaja baadhi ya Sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho, ikiwemo Sheria ya Maliasili.

“Sheria za maliasili zimeendelea kuwa tatizo kubwa Kwa wafugaji Kwa kuweka faini kubwa sana na kuendeleza suala la kuuza mifugo ya wafugaji inayoonekana kukinzana na Sheria za maliasili. Hadi sasa mwaka huu karibu mifugo 10,000 imepigwa mnada na kuwaacha wafugaji katika umasikini. Hili eneo ni kinyume na haki za binadamu ningepen da kusikia maagizo ya Seriksli kusitisha uuzwaji wa mifugo inayipatikana maeneo ya hifadhi badala yake zitolewe adhabu ambazo haziendi kuleta ufukara Kwa wafugaji asili,” amesema Olengurumwa.

Kuhusu hotuba ya Waziri Majaliwa, Olengurumwa amesema “Hotuba ya waziri mkuu ni matumaini makubwa kwa wafugaji asili endapo itafanyuwa kazi kwa ushirikishwaji Mpana na wafugaji wenyewe. Ni ukweli usiopingika kuwa ufugaji wetu wa asili Kwa Sasa unapitia changamoto nyingu ambazo Ingine ziko nje ya uwezo wetu kama mabadiliko ya tabia ya nchi. Serikali imekubali Kuna changamoto ya uhaba was ardhi Kwa wafugajiasili suala hili ndilo kikekuwa kilio cha muda mrefu na likifangiwa kazi huenda ikasaidia kuboresha sekta hii.”

Katika hotuba yake, Waziri Majaliwa alitoa maagizo kadhaa ikiwemo, uboreshwaji wa mikakati ya elimu Kwa wafugaji, mashamba ya NARCO yarudishwe Kwa wafugaji, wafugaji wapewe ardhi ili waache kuzunguka Kila mahali na halmashauri zisimamie kutatua migogoro iliyopo ya wafugaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!