October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Oman yavutiwa kuwekeza Tanzania

Spread the love

SERIKALI ya Oman imevutiwa kuwekeza katika madini ya viwandani na madini ya ujenzi nchini. AnaripotiMwandishi wetu … (endelea).

Kauli hiyo, ameitoa Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saud All-Shidhani baada ya kukutana na Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko leo Agosti 10, 2022 katika Ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi Shidhani amesema Oman imevutiwa kuwekeza kutokana na hali ya utulivu uliyopo nchini, amani, na mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Madini chini ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Dk. Biteko amesema milango ya Wizara ya Madini kwa wawekezaji iko wazi na kuwataka wale wote wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini Tanzania wafike Wizarani hapo.

Aidha, Dk. Biteko amesema Wizara ya Madini inawahitaji wawekezaji kuliko wawekezaji wanavyoihitaji Wizara hiyo ambapo amewaomba waje nchini kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Pia, Dk. Biteko amekutana na kuzungumza na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya almasi ya Williamson Diamond Limited (DWL) kwa lengo la kupata mrejesho wa kikao kilichofanyika awali.

error: Content is protected !!