May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Olengurumwa afikisha kilio kwa Rais Samia

Spread the love

 

ONESMO Olengurumwa, Mratibu Mkazi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, afute zuio la wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito, kurudi shuleni baada ya kujifungua.Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Olengurumwa ametoa ombi hilo leo Jumapili tarehe 23 Mei 2021, katika ziara yake ya kutembelea wadau wa THRDC, mkoani Shinyanga.

Mratibu huyo wa THRDC, ameshauri Serikali ya Rais Samia, irekebishe sheria zinazowakwamisha watoto wa kike kuendelea na masomo, hasa wanaopata ujauzito wakiwa shuleni.

“Tumekuwa tukilalamika kuna sheria zinasababisha changamoto, hizi sheria ziwekwe vizuri ziweze kusaidia watoto wa kike. Mfano binti kurudi shule ni jambo la msingi sana anapopata ujauzito, nadhani Rais Samia tumuombe ahakikishe kwamba binti anapopata changamoto hiyo anarudi shule,” amesema Olengurumwa.

Zuio la wanafunzi wanaopata ujauzito kurudi shuleni baada ya kujifungua, liliwekwa 2017 na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli, ambaye aliagiza wanafunzi hao wajiunge na Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA).

error: Content is protected !!