Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ole Sendeka alitaka Bunge liache kulalamika, lichukue maamuzi
Habari za Siasa

Ole Sendeka alitaka Bunge liache kulalamika, lichukue maamuzi

Spread the love

MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Olesendeka, amelitaka Bunge liache kulalamika kwa maamuzi yake iliyokwisha fanya, badala yake litoe maazimio ya kuwachukulia hatua watu wanaoshindwa kufanyia kazi maazimio yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ole Sendeka ametoa ushauri huo leo Jumatano, tarehe 8 Februari 2023, bungeni jijini Dodoma, akichangia hoja zilizowasilishwa na kamati za kudumu za mhimili huo.

Ametoa kauli hiyo wakati akinukuu maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyoandika katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, yaliyosema viongozi kukubali kufanywa vikaragosi ni dalili ya woga na si dalili ya heshima.

Ole Sendekea aliendelea kunukuu maneno ya Mwalimu Nyerere akisema, mwaasisi huyo wa Tanzania aliandika kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta , viongozi halisi hawapendi kuishiriki na kwamba kujenga mazoea ya kutii viongozi hata katika mambo haramu ni dalili ya uoga na kukaribisha udikteta.

“Nayatumia maneno haya sababu sifurahii kuona Bunge likilalamika juu ya maamuzi ambayo mmekwisha fanya, ningependa tutoke na maazimio kwamba wale walioagizwa wayafanye tuwajue ni kina nani, wanapaswa kusimamia katika sekta hizo na Bunge lielezwe nani hawa wanaokaidi,” amesema Ole Sendeka na kuongeza:

“Sisi tuko hapa kwa niaba ya wananchi, tuchukue hatua kama hatuna mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya waziri mmoja mmoja, dhidi ya mtendaji mmoja mmoja, tuchukue hatua hata kwa wale ambao tuna mamlaka nao ili wawasimamie hawa ambao wamepewa dhamana.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!