May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ole Sabaya akamatwa

Spread the love

 

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya, ametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Kamishena wa Polisi, Salum Hamduni, amethibitisha kukamatwa kwa Sabaya na kuongeza kuwa taasisi yake, inamshikilia mwanasiasa huyo, kwa ajili ya mahojiano.

Anasema, Sabaya anashikiliwa kutokana na kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Hata hivyo, Hamduni hakuzungumzia suala hilo kwa undani. Aliishia kusema, “ni kweli kuwa Takukuru inamshikilia Sabaya, kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi ya madaraka na rushwa, wakati akiwa mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.”

Kwa habari zaidi, soma gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Ijumaa – Mhariri.

error: Content is protected !!