December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ole ‘out’ Ma U, Carrick abeba mikoba

Spread the love

 

BAADA ya mwenendo mbovu wa matokeo ya michezo mbalimbali, uongozi wa Manchester United ya Uingereza umemfungashia vilango kocha wake, Ole Gunnar Solskjaer. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ole aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo miaka ya nyuma yenye maskani yake Old Trafford ametimuliwa leo Jumapili, tarehe 21 Novemba 2021 na nafasi yake inakamiliwa na Michael Carrick.

Carrick ambaye naye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United, alikuwa msaidizi wa Ole ambaye alitua Old Trafford mwaka 2018 akichukua nafasi ya Jose Mourinho.

Ole ametimuliwa ikiwa ni siku moja imepita tangu kushuhudia vijana wake wakipokea kipigo cha 4-1 kutoka kwa Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

error: Content is protected !!