Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Ole Nasha kuagwa kesho Dodoma, kuzikwa Jumamosi Arusha
Tangulizi

Ole Nasha kuagwa kesho Dodoma, kuzikwa Jumamosi Arusha

Spread the love

SERIKALI imesema aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Tate Ole Nasha ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Ngorogoro (CCM ) atazikwa Jumamosi tarehe 2 Oktoba, mwaka huu kijijini kwake kwa matakwa ya familia yake. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea…)

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 Septemba 2021, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema bado wanaendelea na vikao vya maandalizi ya maziko ya kitaifa.

Amesema Serikali inaendelea kuungana na Watanzania wengine kuomboleza msiba wa kiongozi huyo aliyefariki tarehe 27 Septemba, 2021 akiwa nyumbani kwake maeneo ya Medeli jijini Dodoma.

“Kesho siku ya Alhamisi tutafanya buriani ya kitaifa itakayohusisha viongozi wote katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania majira ya saa 5 asubuhi.

“Kwa sasa tunaendelea na vikao vya ndani kati ya Ofisi ya Bunge na sehemu alikokuwa anaabudu marehemu kiimani ili kuona namna tutakavyompa heshima ya mwisho,” amesema Mhagama.

Aidha, ameeleza kuwa baada ya mazungumzo yote marehemu Ole Nasha atapewa heshima za mwisho kisha kuanza safari ya kuelekea kijijini kwake Arusha ambako atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele siku ya Jumamosi.

“Ijumaa na Jumamosi ndiyo siku ambazo zitakuwa za maziko kijijini kwake, hayo ndiyo maamuzi ya kikao chetu cha awali, tutakaa tena saa kumi jioni kuona kama kuna jambo lingine jipya tutawajulisha,kwa sasa ni hayo tu,” amesisitiza Waziri huyo.

Amesema, Serikali kwa kushirikiana na familia ya marehemu Ole Nasha inaendelea kufanya mazungumzo pia na Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho kimemlea ili kufanikisha maandalizi yote muhimu kuanzia hatua za awali hadi mwisho wa maziko.

Aidha, Waziri Mhagama amewashukuru watanzania kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kipindi hiki cha maombolezo huku akiwataka kuendelea kuwa watulivu.

Kwa upande wake msemaji wa familia, Edward Polokwa ameishukuru Serikaki na CCM kwa kuwapa ushirikiano tangu msiba ulipotokea na kwamba familia kwa ujumla imefarijika.

“Tumefarijika sana, Serikali imekuwa bega kwa bega na sisi tangu siku ya kwanza tulipopokea taarifa za msiba wa ndugu yetu,jambo hili limetupa faraja,” amesema Polokwa.

William ole Nasha alizaliwa mwaka 1972 mkoani Arusha ambapo katika uhai wake ameitumikia Serikali katika nyanja mbalimbali ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa akitumikia nafasi ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!