August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Okwi rasmi SC Villa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi

Spread the love

BAADA ya kuvunja mkataba na klabu yake ya SønderjyskE inayoshiriki ligi kuu nchini Denmark, hatimaye mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi amerudi nchini kwao na kujiunga na Sc Villa inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Okwi amejiunga na klabu yake ya Zamani alioachana nayo mwaka 2010, kwa mkataba wa muda mfupi utakao muwezesha kuwepo mpaka mwisho wa msimu huu wa 2016/2017.

Taarifa za mshambuliaji huyo hapo awali zilikuwa zikionesha anarudi nchini Tanzania kujiunga na klabu yake ya Simba, ambao waliomuuza kwenda nchini Dermark, lakini huwenda akarejea baada ya msimu kumalizika kutokana na dirisha dogo la usajili kwa wachezaji lilisha fungwa.

Huwenda huu ukawa mpango mkakati wa klabu ya Simba kumpeleka Okwi kwenye klabu ya SC Villa kwa mkataba wa muda mfupi ili kulinda kiwango chake na baada ya msimu kumalizika aweze kurudi na kujiunga na timu yake ya Simba ambao viongozi wake walishaonesha dalilili ya kutaka kumsajiri.

error: Content is protected !!