July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Okwi arejea Simba, aongeza mzuka

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Uganda na klabu ya Al Ittihad Alexandria, Emmanuel Okwi  ameongeza mzuka kwenye kambi ya Simba iliyopo Cairo nchini Misri, baada ya kuwatembelea wachezaji wa kikosi hiko kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi A, utapigwa leo majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambayo itakuwa mechi ya mwisho kwenye hatua hiyo ya makundi.

Kupitia mitandao ya kijamii ya klabu ya Simba, ilionesha mchezaji huyo ambaye anakipiga kwenye klabu hiyo nchini Misri, aliwatembelea wachezaji hao na kupata nao chakula cha mchana na kuwatakia kila la kheri kwenye mchezo wao wa usiku dhidi ya Al Ahly.

Okwi ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kwa kufika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2018/19.

Simba inaingia kwenye mchezo huo, huku ikiwa tayari imeshafuzu kwa hatua ya robo fainali wakiwa wanaongoza Kundi A, wakiwa na pointi 13.

error: Content is protected !!