Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo
Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the love
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza ofisi zote za mabalozi wa mashina nchini zitumike kuwalea na kuwajenga watoto katika misingi ya maadili ya kitanzania kama njia rahisi ya kuimarisha usalama wao na mali zao. Anaripoti Christina Haule,Ulanga … (endelea).

Chongolo alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM  shina namba tano wilayani Ulanga ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tisa Mkoani Morogoro yenye lengo la kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo.

Chongolo alisema ni vema ofisi za mabalozi na Mashina zikatumika kwa kufanya vikao vya wazazi na watoto wao kubaini changamoto za watoto na vijana na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Aidha alisema wazazi wananafasi kubwa ya kuwalea watoto katika misingi ya Mila na tamaduni walizokulia wao na hivyo kupata vijana bora wasioweza kujiingiza kwenye vitendo viovu ikiwemo kuwaibia wazazi wao.

Aidha aliitaka jamii kufuatilia na kuzingatia elimu inayotolewa bure na Serikali kupitia vyuo vya ufundi stadi VETA hapa nchini kwa vijana ikiwa ni lengo la kusaidia vijana kupata ajira binafsi na kutojiingiza kwenye makundi ya vishawishi vya wizi au udokozi.

“Rais Samia ametenga nafasi kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza masomo ya shule za msingi kuendelea na elimu ya ufundi katika vyuo vyote vya VETA nchini, hata kama wazazi wao hawana uwezo wa kuwapeleka vyuoni” Alisema Chongolo.

Awali katibu wa shina namba tano Raphael  Boma  alisema kumeibuka matukio mengi ya wizi au udokozi wa wanyama wafugwao nyumbani, vyakula na mashambani Mambo yanayofanywa na makundi ya vijana ndani ya wilaya hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!