Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ziara ya Rais Magufuli Iringa, bendera za Chadema zashushwa
Habari za Siasa

Ziara ya Rais Magufuli Iringa, bendera za Chadema zashushwa

Bendera ya Chadema
Spread the love

OFISI za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zilizopo Mafinga, Iringa zimevamiwa. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Tukio la uvamizi huo katika Jimbo la Mbinga, limefanyika usiku wa kuamkia leo Alhamisi tarehe 10 Aprili 2019.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Katibu wa Chadema mkoani Iringa, Jackson Mnyawami amesema, bado haijafahamika watu waliohusika kwenye tukio hilo.

Mnyawami amesema, licha ya watu hao wasiojulikana kuvamia ofisi hizo, waliondoa bendera za chama hicho zilizoko katika maeneo ya Mbalamaziwa, Nyororo, Stendi Kuu ya Mafinga, Njiapanda ya Madibila, Ndolezi na Ifunda.

“Usiku wa kuamkia Alhamisi Aprili 10 2019, kumetokea matukio ya uvamizi wa ofisi ya chama, Jimbo la Mafinga Mjini na kuondolewa bendera.

“Kwa mfano, bendera ya Stendi Kuu Mafinga iko mita 5 kutoka Kituo cha Polisi pamoja na polisi waliopo kituoni hapo na waliopo lindo la benki ya Posta, lakini imeondolewa,” amesema na kuongeza:

“Vitendo hivi vinatokea wakati Rais John Magufuli akifanya ziara mkoani Iringa. Vitendo vya kuvamia ofisi za Chadema ni uvunjwaji wa makusudi wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ni uporaji wa haki za vyama vyote na ubaguzi wa wazi wazi.”

Mnyawami amesema, wameliandikia Jeshi la Polisi barua ya malalamiko yao kuhusu vitendo vya kuondolewa bendera za Chadema.

“WanaCCM wanataka kumuonyesha rais kwamba Iringa hakuna Chadema, hakuna upinzani.

“Tunatoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama, kuchukua hatua dhidi ya wale wote wanaohusika na vitendo hivi, kwani vinaweza kutengeneza chuki ya kisiasa na uhasama wa kisiasa hususani kwa kipindi ambacho mkoa utakuwa na ugeni mkubwa wa Rais,” amesema Mnyawami.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!