Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ofisi ya Msajili: Mkapa ana historia ndani ya CUF
Habari za Siasa

Ofisi ya Msajili: Mkapa ana historia ndani ya CUF

Sisty Nyahoza, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania
Spread the love

SISTY Nyahoza, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania amesema, Hayati Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya tatu ameacha mchango wake ndani ya Chama cha Wananchi (CUF). Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho ulioitishwa kwa ajili ya kupitisha majina ya wagombea urais Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020, Nyahoza amesema, miongoni mwa mambo aliyoanzisha Rais mstaafu Mkapa yaliinufaisha CUF.

Amesema, mwaka 1995, Rais Mkapa alianzisha ruzuku ya chama na kwamba, miongoni mwa vyama vya mwanzo kunufaika na ruzuku hiyo ni CUF.

“CUF ilianza kunufaika na mpango wa Rais Mkapa, lakini tulikuwa na tatizo la siasa Zanzibar, Rais Mkapa ndiye aliyesimamia na kutatua mgogoro huo kwa kusaini mkataba wa marudhiano. Sio hivyo tu, Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar uiliratibiwa na Rais Mkapa ndio maana nasema Mkapa ana historian a CUF,” amesema.

Pia, Nyahoza amesema, mpango wa Viti Maalum mwaka 2005 ulionzishwa na Rais Mkapa, CUF ni miongoni mwa vyama vya mwanzo vilivyonufaika.

Msajili huyo pia ameipongeza CUF kwa dhamira ya kufanya siasa za kistaarabu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

“Naipongeza CUF kwa kuamua kusimamia kauli ya kufanya kampeni kwa ustaarabu. Ninaamini mtasimamia kauli hiyo, lakini pia nampongeza Prof. Lipumba kwa kuandaa mkutano huu,” amesema Nyahoza na kuongeza “CUF bado ipo imara.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!