August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ofisa wa TRA ashikiliwa kwa rushwa

Spread the love

FLAVIAN Chacha (33), Ofisa Kodi Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dodoma ametiwa mbaroni na Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 1,500,000 milioni, anaandika Dany Tibason.

Kwa mujibu wa Emma Kuhanga, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, taasisi hiyo inamshikilia Flaviani kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume cha kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Amesema Flaviani aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mfanyabiashara Jackoson Shirima ili asimchukulie hatua kwa kosa la kusafirisha mzigo wa matofari bila kutoa stakabadhi ya mauzo.

“Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 18 mwezi wa tatu mwaka huu maofisa wa TRA wakiwa katika shughuli zao za kikazi walikamata lori aina ya Mistubish Fuso lililokuwa likiendeshwa na Joshua Charles likiwa na mzigo wa matofari kutoka kwandani kwa Shirima.

“Baada ya kulikagua walibaini kwamba mali hiyo iliuzwa bila kutoa stakabadhi hivyo walimuamuru dereva wa gari hilo kulipeleka TRA kwa hatua zaidi, baada ya gari hilo kukamatwa dereva wa gari hilo alimpigia tajiri yake (Shilima ) ili alete stakabadhi iliyokuwa ikidaiwa na maofisa wa TRA.

“Baada ya mazungumzo marefu kati ya Ofisa wa TRA, Flaviani na mmiliki wa kiwanda cha matofari ambaye ni Shilima, ndipo Flaviani alimtaka mmiliki huyo kutoa faini ya Sh milioni 3.

“Lakini mfanyabiashara huyo alilalamika sana na kutaka apunguziwe faini, Flaviani alikubali kumpunguzia hadi kufikia Sh. 1.5 Milioni kinyume na utaratibu,”amesema.

Kuhanga amesema Shilima alimuomba Ofisa wa TRA ampatie muda wa kutafuta fedha hizo na baada ya kupatiwa muda, alienda moja kwa moja Takukuru na kutoa taarifa ya kuombwa rushwa na Ofisa wa TRA.

Amesema, baada ya kupata taarifa hiyo maofisa wa taasisi hiyo walifanya uchunguzi wa awali ili kubaini kama kuna viashiria vya rushwa na baada ya kujiridhisha ndipo mtego wa rushwa uliandaliwa na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

 

error: Content is protected !!