August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ofisa TRA kortini kwa kuomba rushwa

Spread the love

WATU wawili wamepandishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kwa tuhuma ya kuomba rushwa ili kumsaidia mfanyabiashara kukwepa kodi, anaandika Faki Sosi.

Watu hao ni Amani Mkwizu, Ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Edward Magobera, mfanyakazi katika kampuni ya udalali ya Yona Auction Mart.

Akisoma mashitaka hayo Denis Lukayo, Wakili wa Serikali mbele ya Huruma Shahidi, Hakimu Mkazi amesema kuwa, washitakiwa hao tarehe 19 Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam walitenda kosa la kuomba Sh. 50 milioni kwa Glenn Clark, Mkurugenzi wa Kampuni ya Commercial Seles and Services Tanzania Limeted.

Lukayo ameiambia mahakama kuwa, washitakiwa wengine wawili hawapo mahakamani hapo na kwamba, walihusika kwenye kosa hilo pamoja na waliopo mbele yake.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuomba rushwa ili wampunguzie kodi Clark kutoka Sh. 375 milioni hadi kufikia Sh. 100 milioni.

Shitaka la pili linatokana na watuhumiwa kubadilisha kiwango cha pesa walichoomba na kutoka Sh. 50 milioni na kuwa Sh. 500 milioni.

Shitaka la tatu kwa washitakiwa hao ni kujipa mamlaka ya kupunguza kodi kwa mteja, mamlaka ambayo ni ya mwajiri wao.

Wahitakiwa wote wamekana mashitaka yote matatu, mahakama imewakea wazi ndama ya Sh. 5 milioni kwa kila mmoja.

Upande wa mashikata haujakamalisha upelelezi, kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Mei mwaka huu.

error: Content is protected !!