Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ofisa Chadema apigwa risasi, auawa
Habari za Siasa

Ofisa Chadema apigwa risasi, auawa

Spread the love

LUCAS Lihambalimu, Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro jana usiku tarehe 12 Juni 2019, amepigwa risasi nyumbani kwake na kuuawa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).  

Tumaini Makene, Msemaji wa Chadema kwenye taarifa yake amesema, Lihambalimu ameuawa akiwa nyumbani kwake.

Ameeleza kuwa, Lihambalimu alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake maeneo ya Bonde la Kilombero saa nane usiku, ambao walimpiga risasi na kupoteza maisha yake.

 “Watu wenye silaha walifika nyumbani kwa Lihambalimu , wakagonga wakamtaka atoke nje wanasgida naye. Akiwa wanatafuta upenyo wa kuchungulia kuwajua ni wakina nani, walimfyatulia risasi kichwani na kumuua hapo hapo,” imeeleza taarifa ya Makene.

 MwanaHALISI ONLINE ilimtafuta Wilbroad Mutafungwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro kwa njia ya simu kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa tukio hilo, hata hivyo amesema, hana taarifa hizo kwa kuwa, yupo nje ya ofisi kutokana na matatizo ya kiafya.

Kamanda Mutafungwa aliahidi kutoa mawasiliano ya msaidizi wake, kwa ajili ya kueleza undani wa tukio hilo, lakini hadi taarifa hili inachapishwa hakutuma namba za msaidizi wake.

“Bahati mbaya mimi ni mgonjwa, niko hospitali napata matibabu, nahangaika na huduma za kiafya. Nitakupa namba za msaidizi wangu ambaye utamhoji na kuendelea naye kwa taratibu za kiofisi,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Hata hivyo Makene amesema, Chadema inafuatilia kwa karibu kifo hicho “Tunafuatilia taarifa mbaya kuhusu K/Mwenezi, Jimbo la Malinyi, Morogoro, Lucas Lihambalimu aliyevamiwa nyumbani kwake, kupigwa risasi na kufariki hapohapo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!