August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Odinga: Ni uchaguzi wa kufa, kupona

Raila Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (CORD)

Spread the love

RAILA Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (CORD) amesema uchaguzi ujao ni wa kufa na kupona, anaandika Wolfram Mwalongo.

Odinga amesema dalili za ushindi katika uchaguzi mkuu mwakani zipo wazi na kuwa, siri ya ushindi ni kujiandikisha kwa wingi na kusisitiza ambaye hatakuwa na kadi ya kupiga kura, asipewe chakula.

“Kwanini nasema watu wajiandikishe kwa wingi hii? Ni kwasababu uchaguzi huu utakuwa wa kufa na kupona

“Lazima tuhakikishe kila mtu anatoka nyumbani kwake anakwenda kujiandikisha, tupo wengi sana kama tukijiandisha sote basi tutakuwa na kura nyingi,”amesema Odinga.

Aidha, amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kujiandikisha na wapenzi wao ikiwa ni harakati ya kuubwaga Muungano wa Jubelee unaoongozwa na Uhuru Kenyatta, rais wa nchi hiyo “vijana hakikisheni mnawaandikisha wapenzi wenu.”

Kenya inatarajia kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwakani huku kukitarajiwa mabadiliko makubwa katika Tume ya Uchaguzi ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wapinzani nchini humo kwamba sio huru.

error: Content is protected !!