May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Odinga apimwa COVID-19, alazwa hospitalini

Raila Odinga, Kiongozi wa Upinzani wa Chama cha ODM

Spread the love

 

RAILA Odinga, kiongozi wa chama cha upinzani cha ODM, amefikishwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya na kuchukuliwa vipimo vya corona (COVID-19). Umeeleza mtandao wa The Standard Kenya … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na kaka yake, Oburu Odinga leo Jumatano tarehe 10 Machi 2021, kwamba kiongozi huyo wa upinzani amekwenda hospitali hiyo leo asubuhi.

“Odinga amechukuliwa vipimo vya COVID-19, lakini mpaka sasa majibu yake hayajatoka,” amesema Oburu na kuongeza “amekuwa akilalamika uchovu na maumivu.”

Oburu amesema, mdogo wake alieleza kulalamikia maumivu ambapo aliamua kusitisha ziara yake ya Pwani, alipokua katika eneo la Karen.

Mara baada ya kuchukuliwa vipimo hivyo, kiongozi huyo wa upinzani, hakuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

error: Content is protected !!