January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Obama: Trump hatakuwa rais Marekani

Spread the love

BARACK Obama, Rais wa Marekani amesema anaamini kuwa Donald Trump, mgombea urais wa Chama cha Republican hatakuwa rais wa Marekani. Chanzo BBC.

“Ninaendelea kuamini kwamba Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Obama.

Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, anaongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa Chama cha Republican.

Tayari ameshinda uchaguzi wa mchujo jimbo moja, na anaongoza kwenye kura za maoni Jimbo la South Carolina ambako wafuasi wa Republicans watashiriki uchaguzi wa mchujo Jumamosi.

Akiongea wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia unaofanyika katika Jimbo la California, Obama aliulizwa na mwanahabari kumhusu Trump.

“Watu hawatampigia kura,” amesema Obama, “kwa sababu wanajua kuwa urais ni kazi kubwa.”

“(Kazi hii ) Si kama kuzungumza katika kipindi cha runinga, si matangazo au mauzo ya bidhaa, ni kazi ngumu. Si kazi ya kushawishi watu na kufanya utakalo ndipo utokee kwenye vichwa vya habari siku fulani.”

Trump amemjibu na kusema, “ni kama kusifiwa kutokana na kukosolewa na rais ambaye ameharibu sana nchi.”

Mwanasiasa huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.

error: Content is protected !!