January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Obama kushambulia ISIS kutoka angani

Spread the love

Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza rasmi mvua ya mabomu dhidi ya Dola ya kiislam (ISIS) iliyojitwalia kwa mabavu maeneo ya mipaka ya nchi za Siria na Irani na kuyatangaza maeneo hayo kama himaya yake.

Obama alitoa kauli hiyo Jumatato iliyopita alipokuwa kwenye maazimisho ya miaka 13 tangu mashambulizi ya 11 Septemba 2001. Obama akizungumza kuhusu shambulio hilo alimesema mashambulizi yataelekezwa pia ndani ya Syria.

Obama alisema mashambulizi ya angani ni lazima kama njia ya kudhibiti kundi hilo la kigaidi, ili lisifikie hatua ya kuwa tishio kwa Marekani.

Mpango huu ni lazima uridhiwe na Baraza la Wawakilishi (House of Representative) kwa kupiga kura. Hata hivyo pamoja na mapungufu yaliyopo kwenye mkakati wa mashambulizi haya, uwezekano wa kuunga mkono mpango huu ni mkubwa kwani hata Spika wa chombo hicho John Boehmer amesema anamuunga mkono Rais.

Pamoja na Boehmer kumuunga mkono rais alionyesha wasiwasi na mkakati wake usioonesha ni nini hasa kitafanyika kuweza kuiangamiza ISIS. Boehmer alisema shambulio la angani kwa kutumia F-16 halitoshi, kunahitajika askari wa ardhini pia.

Wakati huohuo ISIS wamesema mashambulizi ya angani hayataweza kuzuia dola ya kiislamu.

Hata waasi wa Syria wanaosaidiwa na Marekani pamoja na wananchi wa Syria ya Kaskazini wameonesha wasiwasi wao kuwa, mkakati huo hautakuwa na mafanikio bali matatizo ikiwa ni pamoja na mauaji ya raia.

Uamuzi wa Baraza la Wawawakilishi la Marekani kupiga kura ya aidha kuunga mkono au kuhusu mpango huo unategemewa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

error: Content is protected !!