Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Obama akipuuza chama chake
Kimataifa

Obama akipuuza chama chake

Barack Obama, Rais wa Marekani anayemaliza muda wake
Spread the love

RAIS Barrack Obama anayemaliza muda wake wa kukaa Ikulu ya Marekani siku ya kesho amepuuza msimamo wa chama chake cha Democtatic  kususia sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule Donald Trump, anaandika Wolfram Mwalongo.

Obama amesema atashiriki kikamilifu zoezi la kumkabidhi madaraka Trump licha ya msimamo wa chama chake wa kususia tukio hilo la kihistoria.

Akizungumza katika mkutano wake wa kuagana na wanahabari aliofanya nao kazi kwa miaka nane, Obama amesema Wamarekai hawapaswi kuwa na hofu kwani Taifa hilo ni la Wamarekani wote.

“Nina imani na nchi yangu na watu wake,” amesema Obama.

Obama ameeleza kuwa kitu alichomshauri Trump ni kushirikiana na wasaidizi wake kwani kazi ya Urais ni kubwa na ngumu.

“Hii ni kazi yenye maana kubwa, hawezi kuifanya peke yake nimeshauri kuwa ni lazima ashirikiane na wasaidizi wake,” amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuitakia heri familia ya George W. Bush Rais wa 41 wa Marekani ambaye amelazwa hospitali pamoja na mkewe Barbara kutokana na matatizo ya kiafya.

Obama pia amedai bado anaamini kuwa upo uwezekano mkubwa Marekani ikaongozwa na rais Mwanamke siku zijazo huku akisema Wamarekani wenye asili ya kigeni waendelea kujitokeza kwenye vinyang’anyiro vya nafasi mbalimbali bila kuhofia chochote.

“Natarajia kuona ongezeko la Wamarekani wenye asili ya mataifa ya kigeni wakiongezeka katika vinyang’anyiro vingi katika pembe zote za Marekani na huenda tukapata rais Mwanamke kutoka huko,” amesema Obama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!