Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Oasis yataja muarobaini tatizo la usugu wa dawa
Afya

Oasis yataja muarobaini tatizo la usugu wa dawa

Spread the love

WANANCHI wametakiwa kutumia vipimo maalumu vinavyoonesha ugonjwa na aina ya matibabu yake sahihi, ili kuepukana na tatizo la usugu wa dawa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Kituo cha Oasis Health Policlinic, kilichopo Mtaa wa Mwongozo, Mabibo Makuburi, jijini Dar es Salaam.

Alizungumza katika uzinduzi huo, Mtaalamu wa Maabara wa Oasis Health Policlinic, Silvin Albert, alisema kituo hicho kinatoa huduma ya kipimo cha Culture and Sensitivity, ambacho kinasaidia kuchambua chanzo cha ugonjwa na matibabu yake.

“Tatizo la usugu wa dawa ni tatizo ambalo linakuwa kwa kasi sana, kwa kuzingatia hayo kama Oasis Labatory tumeamua kutumia mashine za kisiasa zinazo tupa majibu ya uhakika zaidi, kuliko kutumia njia za kawaida. Kwa kutumia mashine tunategemea majibu yetu kuwa ya uhakika ili kumsaidia mgonjwa,” alisema Albert.Mtaalamu huyo wa maabara alisema, madhara ya usugu wa dawa ni mgonjwa kushindwa kupona maradhi yake.

“Madhara yanayotokana na usugu wa dawa ni kwamba, itakusababishia kutumia dawa nyingi na mwisho wa siku hakutakuwa na dawa itakayoweza kukusaidia. Wadudu ambao wako mwilini wameshatengeneza usugu, hizo dawa nyingine zisikusaidie tena, ni sahihi kupata dawa inayoweza kukusaidia kupona kabisa na hiyo inatolana na kufanya kipimo kinachoitwa Culture and Sensitivity,” alisema Albert.

Wakati huo huo, Albert alisema kituo hicho kina mashine za kupima magonjwa zaido ya 100, ikiwemo ya figo, ini, ubora wa mbegu za kiume, viashiria vya kansa, homoni za kike na kiume.

“Tunafanya vipimo mbalimbali ukianza na vipimo vya kawaida, kupima mkojo malaraia na vipimo vikubwa kama kupima ini, figo, kuangalia mafuta mwilini kwa maana ya corestral. Pia tunapima vipimo vya culture and sensitivity,” alisema Albert.

Naye Kimu Mkurugenzi Mtendaji Oasis Health Policlinic, Joan Katula Makoy alisema azma ya kuanziahwa kituo hicho ni kusogeza huduma ya afya karibu na wananchi, ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, za utoaji huduma bora za afya.

“Lengo kuanzisha Oasis Health Policlinic ni kusogeza huduma ya afya karibu na wananchi kwa gharama nafuu, ikiwa lengo ni kuunga juhudi za mama Samia za kuwafikishia huduma za afya wananchi kwa gharama nafuu hasa wananchi wanyonge,” alisema Makoy.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitamile, alisema uanzishwa wa kituo hicho katika mtaa wake, utasaidia wananchi kuoata huduma ya afya kwa haraka.

“Hii huduma iko katikati ya eneo la makazi ya watu, kwa hiyo faida kubwa ya kwanza ambayo tutanufaika nayo ni kutokuwa na umbali, unavyojua Dar es Salaam kuna changampto kubwa ya usafiri wa magari, lakini kituo kiko hapa karibu kutoka majumbani na kufikia huduma ilipo,” alisema Ngoitamile na kuongeza;

“Vilevile kunaonekana kuna vipimo vya hali ya juu, watu wengi na magonjwa mengi yatapimwa hapa. Wananchi natoa wito waje wakitumie kituo chao, kiko nyumbani waje kwa wingi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!