
SERIKALI imepanga kutumia ndege ya kunyunyuzia sumu ili kuangamiza wadudu waharibifu aina ya nzige katika wilayani Longido na Simanjiro. Aanaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Kauli hiyo imetoewa na Profesa Adolf Mkenda, Waziri wa Kilimo jana Jumapili, tarehe 21 Februari 2021, alipotembelea eneo lililovamiwa na wadudu hao wilayani Longido.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, ilitangaza kuandaa vikosi viwili kukabiliana na nzige hao walioingia Tanzania katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Akizungumzi kuhusu ndege hao waharibifu, Prof. Mkenda amesema, tayari Dk Efrem Njau, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kudhibiti Visumbufu (TPRI) na wataalamu wake wapo wilayani Simanjiro na Longido kwa kazi hiyo.
Amewataka wananchi na wakulima kutokuwa na hofu kuhusu nzige hao, kwamba wataangamizwa chini ya uratibu wa Wizara ya Kilimo.

Pia ametahadharisha kwamba, pale wananchi watakapoona nzige wameanguka chini ama wamekufa, wasiwatumie kama chakula kwa kuwa watakuwa na sumu.
“Wananchi wakiona nzige wameanguka chini wamekufa wasiwachukue au kula kwa kuwa wengi watakuwa wamekufa kwa sumu,” amesema Prof. Mkenda.
Imeagizwa kwamba, shule zote zilizopo kwenye maeneo ambayo nzige hao wataangamizwa, zisitishe mazomo kwa siku nne.
Kauli hiyo imetolewa na Jumaa Mhina, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, akilenga watoto kutopata madhara kwa kushika ama kuchezea nzige watakaokufa.
More Stories
Bosi Tarura aagiza ujenzi daraja Kaseke, 1.5 milioni zirejeshwe
Operesheni Samia yawapatia vijana 45,047 mafunzo JKT
Marekebisho sera ya elimu, mitaala kukamilika Desemba 2022