October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nyumba ya mchezaji wa Simba kupigwa mnada

Emmanuel Gabriel

Spread the love

 

KAMPUNI ya udalali ya Greenlight kwa idhini ya Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Kinondoni kituo cha Ukonga, jijini Dar es Salaam, itaiuza nyumba ya mchezaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel Mwakyusa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Nyumba hiyo ya mshambuliaji huyo wa Simba ipo Kitunda jijini humo, itauzwa tarehe 22 Oktoba 2021 kuanzia saa 8:00 mchana.

Ni baada ya Anna Abeid Salum, kushinda madai namba 91/2018 mahakamani hapo.

Tangazo kwa umma lililotolewa leo Jumatano, tarehe 13 Oktoba 2021 na kampuni hiyo ya udalali inaeleza masharti yatakayotumika bila kuathili masharti yaliyopo katika tamko la kuuza.

“Wanunuzi wote watatakiwa kuzingatia vigezo na masharti watakayopatiwa na dalali wa mahakama wakati wa mnada. Ukaguzi wa mali unaruhusiwa kuanzia tarehe ya tangazo kutoka,” linaeleza tangazo hilo

error: Content is protected !!