July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nyumba ya Kamisha yalipuliwa Z’bar

Spread the love

UTABIRI wa machafuko kuelekea uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar sasa umeanza kutimia, anaandika Mwandishi Wetu.

Habari kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba, nyumba ya Hamdani Omar Makame, Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar tayari imelipuliwa kwa mabomu.

Habari hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata watu waliohusika kwenye tukio hilo.

“Kuna watu wamekamatwa kwa kuhisiwa kuhusika na tukio hilo, bado hali sio shwari mpaka sasa,” anaeleza mwandishi wa habari hizi visiwani humo.

Tukio hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo tayari Chama cha Wananchi (CUF), viongozi wa dini, wanasiasa na wanaharakati tayari wametoa tahadhari ya kutokea kwa matukio hayo.

Taarifa zaidi zitakujia baadaye …

error: Content is protected !!