Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia
Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris
Spread the love

 

KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea nyumba ambayo aliwahi kuishi yeye na babu yake miaka ya 1960, jambo ambalo limesababisha kuwapo msako wa nyumba hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, akinukuu gazeti la Times la Uingereza … (endelea).

Bi. Harris, ambaye yuko katika ziara ya siku tisa katika nchi tatu za Afrika, ana mpango wa kuitembelea Zambia mwishoni mwa juma.

Tayari maafisa wakuu 18 wa Marekani wamezuru bara hilo tangu mwezi Januari mwaka huu.

Aliwahi kumtembelea babu yake nchini Zambia wakati akiwa mtoto, babu yake alikuwa mtumishi wa umma wa India ambaye alitumwa huko kusaidia kuwarejesha wakimbizi baada ya taifa hilo kupata uhuru.

Ubalozi wa Marekani mjini Lusaka, umenukuliwa na gazeti la The Times ukiomba umma kusaidia kutafuta nyumba hiyo ya zamani ya Gopalan wakati ambao Bi Harris anataka kuhusianisha enzi za utoto wake na nchi hiyo.”

Taarifa kutoka ndani ya ofisi yake zinasema, safari ya makamu huyo wa rais katika bara la Afrika inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa Marekani katika bara hilo, hasa katika eneo la “usalama na ustawi wa kiuchumi.”

Mwanasiasa huyo aliwahi kutembelea Afrika, wakati akiwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani. Mapema mwakani, Rais wa Marekani, Joe Biden, anatarajiwa kuwa na ziara kama hiyo barani humo.

Mfulululizo wa ziara hizi kwa viongozi wakubwa katika utawala wa Marekani unaonyesha mwamko unaokua kwamba taifa hilo kubwa ulimwenguni, linahitaji kuimarisha ushirikiano wake na bara hilo.

Haya yote yanakuja katika namna ya ushindani unaokuwa kutoka kwa mataifa mengine yenye nguvu duniani, hasa China na Urusi.

Kabla ya kutembelea Zambia, Harris ambaye atakuwa na ziara ya siku tisa Afrika, atatembelea Ghana kabla ya kuja Tanzania.

Ghana, inayowekeza kuimarisha uhusiano na watu wanaoishi nje ya Afrika na vile vile ikiwa na rekodi ya kubadilishana madaraka kwa njia kidemokrasia na amani, inatoa fursa bora kwa Harris kuanza kuitembelea.

Safari yake, kulingana na taarifa rasmi, itagusia kuhusu mkutano ujao wa kilele wa Desemba kati ya Marekani na Afrika, unaotarajiwa kufanyika huko Washington ambapo Rais Biden alisema, taifa lake limejikita katika mustakabali wa Afrika.”

Wakati ziara ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, huko Ethiopia na Niger, taifa hilo liliangazia matatizo ya usalama yanayoikabili nchi hizo; ziara ya makamu wa rais itaweza kumfikisha katika mataifa yanayokabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Uchumi unaostawi wa Ghana unapitia kwenye wakati mgumu zaidi wa kifedha katika miongo kadhaa.

Nchi hiyo inayohaha kulipa deni lake la taifa, inakabiliwa na mfumuko wa bei wa zaidi ya asilimia 50. Waziri wa Fedha Ken Ofori-Atta amekuwa Beijing hivi karibuni akiongoza mazungumzo na serikali ya China.

“Hadi sasa, mikutano chanya na ya kutia moyo sana imefanyika nchini China,” waziri wa fedha aliandika kwenye mtandao wake wa twitter huku akionyesha matumaini kwamba nchi hiyo itapata usuluhishi “hivi karibuni.”

Haijabainika ni eneo gani kama msaada, Bi Harris anaweza kutoa, lakini ziara yake itakuwa chini ya shinikizo la kufanya kitu kama mshirika aliye tayari kusaidia hasa kufuatia ziara ya Ofori-Atta nchini China.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

error: Content is protected !!