May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyumba 19 zateketea kwa moto Rufiji

Spread the love

 

NYUMBA 19 zimeteketea kwa moto katika kitongoji cha Shaurimoyo, kijiji cha Nyamwage wilayani Rufiji mkoani Pwani baada ya mwananchi mmoja kuwasha moto kwa lengo la kusafisha shamba lake. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo Agosti 30, limethibitishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge.

Kunenge ambaye aliambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Rufiji wamefika kwenye eneo la tukio na kufafanua kuwa mbali na makazi ya wanakijiji kuharibiwa hakuna mwananchi aliyepoteza maisha kutokanaa na moto huo.

error: Content is protected !!