October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyuklia yazidi kumtesa Rais Trump 

Spread the love

RAIS wa Marekani Donald Trump amesaini sheria mpya ya kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini juu ya mpango wake wa zana za Nyuklia kwa madi kwamba ni hatarishi kwa usalama wa taifa lake, anaandika Catherine Kayombo.

Kupitia Waziri wa Fedha wa Marekani, Trump ameidhinisha vikwazo hivyo  dhidi ya makampuni ya fedha yanayofanya biashara zake ndani ya Korea Kaskazini.

Ikiwa ni njia mojawapo ya kuyumbisha uchumi wa nchi hiyo katika biashara yake ya Nyuklia, rais wa Marekani amesema kuwa benki kuu ya China imeagiza taasisi za fedha kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.

Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la Umoja wa Mataifa (UN) kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo kwa sababu ya jaribio lake la hivi karibuni la makombora ya masafa marefu.

Kufuatia jaribio hilo, hali ya wasiwasi imeendelea kutanda hasa nchini Marekani ambako majaribio kadhaa ya mwanzo yalielekezewa huko.

error: Content is protected !!