February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nyufa Hostel za Magufuli zaanza kurekebishwa

Spread the love

SIKU chache baada ya kusambaa kwa picha zilizoonesha nyufa katika kuta za majengo ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), nyufa hizo zimeanza kukarabatiwa, anaandika Mwandishi Wetu.

Ukarabati huo unafanyika na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo Desemba 3, mwaka huu picha za nyufa hizo zilisambaa mitandaoni huku Kumbusho Dawson, Mbunge katika serikali ya wanafunzi UDSM (Daruso) alishikiliwa kuhojiwa na baadaye kuachiwa huru na polisi kitengo cha makosa ya mtandao.

Hata hivyo TBA ilitolea ufafanuzi nyufa hizo kupitia Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga na kueleza kuwa kutokea kwa nyufa hizo ni jambo la kawaida na haina madhara.

Majengo hayo ambayo yalijengwa na TBA ambao wameeleza kuwa bado inaangalia dosari nyingine zilizopo katika majengo hayo.

error: Content is protected !!