August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyota ya Kafulila yaanza kung’ara

Spread the love

DAVID Kafulila, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi) na ambaye amefungua shauri mahakamani kupinga kutangazwa kwa Husna Mwilima, kuwa mbunge wa jimbo hilo, ameanza kupata ushindi katika shauri lake, anaandika Pendo Omary.

Ni baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora chini ya Jaji Ferinand Wambali leo kuridhia maombi yake ya kuwasilishwa mahakamani hapo, fomu halisi za matokeo ya uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kafulila alikuwa ameiomba mahakama kuiamrisha NEC kuwasilisha fomu hizo mahakamani ili ziweze kupitiwa kwa kulinganishwa na fomu alizowasilisha mahakamani.

“Hiki kilikuwa kizingiti kigumu sana. Lakini tunamshukuru Mungu tumekivuka. Uamuzi wa mahakama wa kuiagiza NEC iwasilishe fomu halisi za matokeo, imerahisisha kazi yetu ya kudai haki,” ameeleza mmoja wa wafuasi wa Kafulila, nje ya mahakama mjini Kigoma.

Katika shauri hilo, Kafulila anatetewa na wakili mashuhuri nchini, Prof. Abdallah Safari.

Awali Kenned Fungamtama na wakili wa serikali walipinga maombi ya Kafulila.

Fungamtama anamtetea mshitakiwa wa tatu ambaye ni Mwilima, aliyetangazwa mshindi kwa kile ambacho Kafulila “ubakaji wa demokrasia”.

Wakili wa Serikali anamtetea mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mshitakiwa wa pili ambaye Msimamizi wa uchaguzi

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika 25 Oktoba, inadaiwa kuwa Kafulila ndiye aliyeibuka kidedea. Lakini msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea huyo wa CCM, badala ya Kafulila.

error: Content is protected !!