Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Michezo Nyota watatu wa Arsenal waongeza mkataba
Michezo

Nyota watatu wa Arsenal waongeza mkataba

Spread the love

WACHEZAJI wa klabu ya Arsenal Oliver Giroud 30, Laurent Koscielny 31 na Francis Conquelin 25, wameongeza mikataba yao ndani ya timu hiyo na kuendelea kuitumikia timu hiyo katika michuano tofauti.

Licha ya klabu ya Arsenal kutoweka wazi urefu wa mikataba hiyo, lakini Laurent Koscielny ambaye ni mmoja wa wachezaji waliosaini makubaliano mapya leo, aliandika kwenye ukurasa wake kupitia mtandao wa twitter kuwa ataendelea kusalia ndani ya timu hiyo mpaka 2020.

Nae kocha wa klabu hiyo Arsenal Wenger hakuwa nyuma kuwazungumzia wachezaji wake hao watatu kuwa wamekuwa na uzoefu kwa sasa na ni habari nzuri kwao baada ya kuongeza mkataba.

“Francis amepiga hatua kubwa kiufundi ndani ya uwanja, Olivier anauzoefu wa kutosha na Laurent amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi chetu na naamini ni beki bora kwa sasa ulimwenguni” Wenger alisema.

Arsenal ambayo ipo nafasi ya tano kwenye ligi kwa sasa, inapitia katika kipindi kigumu kutokana na nyota wake Alexis Sanchez na Mesuit Ozil kutaka kuongezewa mshahara ili waendele kusalia kwenye kikosi hicho kutokana na mikataba yao kuwa ukingoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!