March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nyota sita Spurs kuikosa Barcelona

Spread the love

KLABU ya Tottenham Hotspur ya Uingereza itawakosa wachezaji wake sita wa kikosi cha kwanza kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Barcelona utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Wembely, London. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Wachezaji watakaoukosa mchezo huo wa kundi B ni Dele Alli, Mousa Dembele, Serge Aurier, Hugo Lloris, Christian Eriksen na mlinzi wa kati Jan Vertonghen ambao ni majeruhi.

Aurier ataendelea kukosekana baada ya kusumbuliwa na msuli wa nyuma ya mguu huku Dele Alli na Vertonghen wote watakuwa nje baada nao kupatwa na tatizo la misuli katika mchezo wa Ligi Kuu wiki iliyopita dhidi ya Huddersfield.

Kukosekana kwa wachezaji hao muhimu wa kikosi cha kwanza kwenye unaweza ukawa mtihani mgumu kwa kocha mkuu wa timu hiyo Mauricio Pochettino mbele ya mabingwa hao wa La Liga ambao nao hawakuwa na matokeo mazuri katika michezo miwili ya ligi iliyopita.

Spurs ambayo inakwenda kuvaana na Barcelona huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mchezo wao uliopita dhidi ya Inter Milan ya Italia, na kufanya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo huku ikiwa haina alama yoyote.

error: Content is protected !!