November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyoni awaita mashabiki wa Simba Uwanjani

Spread the love

 

MCHEZAJI kiraka wa klabu ya simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Erasto Nyoni, amewataka mashabiki wa klabu ya Simba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kuwa wamejiandaa vizuri kuwapa furaha siku hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utapigwa siku ya Jumamosi tarehe 11 Disemba, 2021 majira ya saa 11 jioni kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Nyoni amesema hayo ikiwa imesalia siku moja kabla ya mafahari hao kuumana kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara toka kuanza kwa msimu mpya wa 2021/22.

Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa klabu hiyo, Nyoni amesema kuwa anaamini mchezo huo utakuwa wa kuvutia kwa kuwa kila timu inahitaji alama tatu, licha ya wao kujiandaa vizuri Zaidi kuondoka na alama hiyo.

“Tumeanza maandalizi yetu salama kucheza na watani zetu jumamosi, naamini utakuwa mchezo mzuri na wakuvutia, sisi tumejianda na tunajindaa kuondoka na pointi tatu.” Alisema mchezaji huyo

Umuhimu wa mchezo huo unakuja kufuatia kuachana kwa pointi mbili kwenye msimamo wa Ligi mara baada ya kuchezwa michezo saba.

Yanga wapo kileleni wakiwa na pointi 19, huku nafasi ya pili ikishikwa na Simba wakiwa na pointi 17, wote wakiwa hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Aidha mchezaji huyo aliendelea kwa kuwataka mshabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuipa sapoti timu yao.

“Naomba wanasimba wajitokeze kuipa sapoti timu yao waewe na imani na sisi, mashabiki wetu waje kwa wingi kuujaza uwanja na kupata furaha.” Alisema Nyoni

Kama Simba itashinda kwenye mchezo huo, Simba itapaa moja kwa moja kwenye msimamo wa Ligi kuu kwa kufikisha ponti 20 na Yanga kusalia kwenye nafasi ya pili.

Kwa upande wa Yanga umuhimu wa mchezo huo unakuja kutokana na uhitaji wa alama hizo tatu ili kuendelea kuwaacha mbali wapinzani wao hao wa karibu.

 

error: Content is protected !!