August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyongeza mishahara kuikutanisha Serikali, TUCTA

Rais Jakaya Kikwete akiwa meza kuu na viongozi wengine wa serikali na TUCTA

Spread the love

SERIKALI inatarajia kukutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kwa lengo la kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Hatua hiyo inakuja baada ya kuibuka kwa mjadala kuhusu kiasi kilichoongezeka katika mishahara ya watumishi ya Mwezi Julai kuwa kidogo tofauti na matarajio ya wengi baada ya Serikai kuongeza kima cha chini kwa asilimia 23.3.

Kupitia ukurasa wa twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewataarifu wafanyakazi kuwa Serikali itakutana na viongozi wao Jumanne tarehe 26 Julai, 2022. Hata hivyo taarifa hiyo haijaeleza ni wapi watakapokutania.

“Ndugu wafanyakazi, Jumanne tarehe 26 Julai, 2022 Serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) ili kusikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai, 2022,” imesema taarifa hiyo.

error: Content is protected !!