August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyerere, Nkuruma, Lumumba ndio marais bora – Askofu

Spread the love

MWALIMU Julius Nyerere wa Tanzania, Nkwame Nkuruma wa Ghana na Patrice Lumumba kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) ni miongoni mwa marais wa kipekee waadilifu Afrika, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa jana na Dk. Barnabas Mtokambali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Asembless of God (TAG) wakati wa mahubiri ya uzinduzi na uwekaji jiwe la msingi wa Kanisa la Jerusalem Christian Centra (JCC) Tanzania Assembile of God lililopo Nkuhungu mjini Dodoma.

Askofu Mtokambali amesema, kwa muda mrefu viongozi hao katika Bara la Afrika akiwemo Nelson Mandela wa Afrika Kusini ndio waliweza kuongoza nchi zao kwa uaminifu na bila kuutukuza wizi na ulaghai.

Dk. Mtokambali akihubiri kanisani hapo kwa lengo la kusisitiza uaminifu kwa viongozi amesema, ni vyema wakaiga mifano ya viongozi hao ambao waliongoza nchi zao kwa uaminifu mkubwa katika maeneo yao katika kipindi chao.

Licha ya kuwataja viongozi hao amesema kwa sasa Mungu ameiona nchi ya Tanzania kwa kuipatia Rais John Magufuli kuiongoza nchi ambayo ilikuwa inanuka uozo mkubwa na ufisadi wa kutosha.

Amesema, kitendo cha Rais Magufuli kupata nafasi hiyo ya urais kwa sasa anaweza kuongeza idadi ya viongozi waaminifu kufikia wane.

Amesema, kwa kipindi kirefu Tanzania imekuwa ikiongozwa na watu ambao siyo waaminifu ambao walipenda kujilimbikizia mali bila kujali kuwa, wapo watu ambao wanataabika kwa umasikini walionao.

“Katika eneo hili tumeweza kuwa na marais watatu tu ambao waliweza kuweka historia ya kuongoza kwa uaminifu waliobaki wote walikuwa ni wezi na wanyang’anyi kwa kupenda kujilimbikizia mali bila kujali shida za wananchi.

“Hata kwa Tanzania kwa kipindi kirefu tumekuwa na viongozi ambao hawakuwa na haja ya kuwa sikiliza watu wanyonge.

“Rais Magufuli amekuwa mwaminifu mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha anasimamia kile ambacho anaona kitakuwa ni haki kwa Watanzania wengi huku akiwashukia vigogo ambao walikuwa wakijilimbikizia mali,” amesema Askofu Mtokambali.

error: Content is protected !!