June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyerere aenziwa kwenye changamoto

Mwenyekiti wa Programu ya Uongozi na Maadili, Pius Msekwa akizungumza kwenye uzinduzi huo

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete amezindua Program maalumu ya uongozi na maadili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambacho kinadaiwa kukabiliwa na changamoto lukuki. Anaandiaka Sarafina Lidwino … (endelea).

Makamu mkuu wa chuo hicho, Prof.Shedrak Mwakalila amesema, licha ya chuo kuendelea kupanuka kwa kuongeza matawi nchini pamoja na kuzindua mtaala mpya wa uongozi na maadili, bado kinakabiliwa na changamoto kubwa.

Mwakalila ametaja changamoto hizo kuwa ni, tatizo la uhaba wa hosteli – kampasi ya Kivukoni na Zanzibar, ufinyu wa bajeti, ambao unaathiri utekelezaji wa majukumu mbalimbali, kushindwa kuongeza vifaa vya kufundishia na mmomonyoko wa ardhi ufukweni mwa bahari ambao unatishia kuangusha baadhi ya majengo.

“Tunaomba ujio wako Rais uwe chachu ya kupatikana kwa suluhisho la changamoto tulizoziainisha, ni matarajio yetu kuwa Serikali itatoa ushirikiano ili kutekeleza azma ya chuo katika kutoa  mafunzo ya uongozi  na maadili, kwa kuleta viongozi bora,” amesema Mwakalila.

Katika uzinduzi huo, kimeanzishwa kisanduku maalum “Kibweta” ambacho kitakuwa na mkusanyiko wa kumbukumbu mbalimbali vyenye historia ya hayati Mwalimu Nyerere kwa lengo la kuendelea kumuenzi.

Rais Kikwete wakati wa uzinduzi huo, alimsimika rasmi Makamu mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa kuwa mwenyekiti wa program hiyo ya “Kibweta”akisema serikali imeunga mkono kuanzishwa kwa mtaala huo na kwamba itakuwa bega kwa bega kuhakikisha wanafanikiwa katika uendeshwaji.

Ameahidi kuchangia fedha kadhaa za kuendeleza program hiyo yenye lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere, mara baada ya kupata taarifa kamili za kiasi kilichopungua kwenye ujenzi pamoja na kuagiza taasisi mbalimbali kutatua tatizo ka mmomonyoko wa ardhi.

“Nimefurahishwa sana na maamuzi yaliyofanywa na uongozi wa chuo, kuanzisha kitu kama hiki chenye manufaa kwa jamii nzima. Kiongozi bora ni yele anayefata maadili na kuwa mzalendo, na wote waliopitia chuo hiki wako hivyo nikiwepo na mimi mwenyewe,” amesema Kikwete.

Naye Msekwa amesema, amefurahishwa na uteuzi uliofanywa na uongozi wa chuo wa kumchagua katika watu wengi wenye hadhi kuliko yeye, hivyo amewaahidi kuitendea vema nafasi hiyo.

“Kwanza nilivyofikishiwa ujumbe wa kunitaka kuwa mwenyekiti wa Kibweta, nilifurahi sana na hadi sasa nimefurahi, Mwalimu alikuwa rafiki yangu wa karibu, namfahamu vizuri naye alinifahamu. Sasa naweza kusema kitengo kimefika mahali pake,” amesema Msekwa.

error: Content is protected !!