IDARA ya haki ya Marekani inachunguza nyaraka za siri zinazodaiwa kupatikana katika ofisi ya zamani ya Rais Joe Biden, Ikulu ya Marekani inasema. Yameripoti mashirika ya kimataifa … (endelea).
Takriban mafaili 10 kati ya nyaraka hizo zilikutwa zimefungiwa mahali katika Kituo cha Penn Biden huko Washington mnamo Novemba na timu ya wanasheria ya Biden, alisema wakili wake.Nyaraka hizo zimekabidhiwa kwa Hifadhi ya Taifa.
Mtangulizi wa Biden, Donald Trump, na yeye anakabiliwa na uchunguzi wa kupeleka faili za siri Florida baada ya kumaliza urais wake.
Kwa mujibu wa CBS News, FBI inahusika katika uchunguzi wa nyaraka za siri zilizopatikana katika Kituo cha Penn Biden, na Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland ametakiwa kupitia nyaraka hizo.
Chanzo kinachofahamu suala hilo kiliiambia CBS News kuwa nyaraka hizo hazikuwa na siri za nyuklia na zilikuwa zimewekwa kwenye sanduku lenye karatasi zingine ambazo hazijaainishwa.
Richard Sauber, wakili maalum wa Rais Biden, alisema katika taarifa kwa CBS Jumatatu kwamba faili ziligunduliwa kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula na mawakili wa Biden ambao walikuwa wakihamisha vitu.
Biden aliweka ofisi hiyo katika jumba ambalo ni kama maili moja kutoka Ikulu ya White House, akiwa hapo kuanzia mwaka 2017 hadi 2020.
Trump aliandika Jumatatu kwenye mtandao wa kijamii, Truth Social, akiuliza: “Ni lini FBI itavamia nyumba nyingi za Joe Biden, labda hata Ikulu ya Marekani?”
Leave a comment