
Yoweri Museveni
NYARAKA za ushahidi zimeongeza mahakama katika harakati za kuhakikisha, matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyompa ushindi Rais Yoweri Museveni wa Uganda, yanafutwa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).
Tayari mawakili wa Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) wamewasilisha ushahidi zaidi katika mahakama ya juu zaidi nchini humo, kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
Upande wa mawakili wa Rais Museveni tayari umepokea nakala ya mashtaka, Alhamisi wiki hii wanatarajia kufika katika mahakama ya juu kupanga siku ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, katika kipindi cha siku 45 kulingana sheria ya uchaguzi nchini humo.
Kesi hiyo ipo mbele ya jopo la majaji likiongozwa na Jaji Mkuu, Alfonce Owiny Doro.
Hatua ya kuongeza ushahidi huo, imetokana na mawakili wa Bobi Wine kuiomba mahakama kuongeza ushahidi zaidi, ili kuhalalisha ombi lao la kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Januari mwaka huu.
Rais Museveni alitajwa kupata asilimia 58.08 huku Bobi Wine akipata asilimia zaidi ya 35, matokeo yanayopingwa vikali na Bob Wine.
More Stories
Mwanafunzi apeleka kuku shuleni kama malipo ya karo
Goodluck Jonathan kuwania urais tena
Hospitali yakanusha madai maiti ya msanii kuimba Ekwueme usiku