Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Nyamapori kuanza kuuzwa buchani, TAWA wapunguza bei
Habari Mchanganyiko

Nyamapori kuanza kuuzwa buchani, TAWA wapunguza bei

Spread the love

WIZARA ya Maliasili na Utalii imepunguza bei za wanyama wa mbegu kwa asilimia 90 ili wananchi waweze kumudu gharama za ufugaji wanyamapori katika mashamba, ranchi na bustani za wanyamapori na kuwezesha kuwa na uhakika wa kupatikana nyamapori. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki alisema hayo wakati akiongea kwenye warsha ya kutangaza maeneo rasmi ya kuanzisha bucha za nyamapori iliyofanyika makao makuu ya ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA iliyopo mjini hapa.

Dk. Nzuki alisema kupungua kwa gharama hizo kutasaidia wananchi kumudu gharama za ufugaji kwa kuwa ufugaji wa wanyamapori ndio chanzo kikuu cha nyama itakayouzwa kwenye mabucha.

“Kwa mfano bei ya wanyamapori kama nyati imepungua kutoka Sh. 4.1 milioni hadi 210,000, Swala pala kutoka 300,000 hadi 90,000,” alisema Katibu mkuu huyo.

Alisema vyanzo vingine vya upatikanaji wa nyamapori ni pamoja na uwindaji wa kitalii na uwindaji wa wenyeji na wageni wakazi ambapo uwindaji wa kitalii mara nyingi huchukua vitu mbalimbali na nyama zikabaki ambazo zitafikishwa kwa wananchi kupitia mabucha yanayoanzishwa.

Dk. Nzuki alisema mikoa 23 kati ya 26 iliyopo Tanzania itaanza kutoa huduma za mabucha ya nyamapori ambapo mikoa mitatu ya Songwe, Mara na Rukwa itaongezeka baada ya kukamilika utaratibu wa kiutendaji.

Hata hivyo alisema Wizara imeweka vigezo vya magari maalum yatayotumika kama bucha maalum za kubeba na kuuzia nyamapori (mobile butcher) ambayo yatapatiwa leseni za kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa nyama kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Dk. Nzuki alisema mpaka sasa wamepokea jumla ya maombi 25 ya watanzania wanaokusudia kuanzisha bucha za nyamapori ambayo yatapitiwa na kamati maalum ambayo inatarajia kukutana oktoba 12 mwaka huu na kutoa leseni za uanzishaji wa mabucha hayo.

Alisema uanzishwaji wa mabucha hayo ni tafsiri ya sera za nchi katika kutafsiri ya ilani ya CCM ambapo wananchi wanatakiwa kunufaika na rasilimali zilizopo kupitia sura namba 283 ya sheria ya uhifadhi wa wanyamapori.

Naye Naibu Kamishna wa uhifadhi huduma za utalii na biashara (TAWA), Imani Nkuwi alisema TAWA imewaonya wote wanaofikiria kuanzishwa kwa biashara ya bucha za nyamapori kuwa ndio njia ya kufanya ujangili wasifikirie hivyo bali watambue kuwa TAWA imejipanga kudhibiti na kusimamia suala hilo kisheria.

Alisema suala la uanzishaji mabucha ya nyamapori lilikuwepo tangu zamani kwenye miaka ya 1988 chini ya kampuni ambapo lilihamishiwa idara ya wanyamapori Wizarani na kuendelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na kusitishwa mwaka 1989 baada ya kuwepo kwa ujangili mkubwa.

2 Comments

  • Tunatumia gharama kubwa kunyunyiza sumu kuua ndege waharibifu wakati ndege hizohizo tungeuza tukapata pesa za kigeni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!