April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nyalandu, wenzake waachwa kwa masharti

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Singida limewatoa mahabusu Lazaro Nyalandu na wenzake wawili, David Jumbe na mmoja aliyetajwa kwa jina la Samson, kwa dhamana pia kutakiwa kuripoti kesho asubuhi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, Nyalandu, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na wenzake, wameachwa leo tarehe 28 Mei 2019 ikiwa ni siku moja tangu walipowekwa mahabusu na jeshi  hilo baada ya kukamatwa katika mkutano wa ndani wa chama hicho kwenye Kata ya Itaja, Singida.

Taarifa ya Makene inaeleza kwamba, Nyalandu na wenzake wameachwa kwa dhamana yenye masharti kwa kila mmoja kudhaminiwa na watu wawili na amana ya kiasi cha Sh. 5 milioni kwa kila mdhamini.

Nyalandu ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kujivua uanachama wa CCM na kutimkia Chadema, pia wenzake wametakiwa kuripoti polisi mkoani Singida kesho tarehe 29 Mei 2019 saa tatu asubuhi.

Aidha, taarifa ya Makene imesema Jeshi la Polisi mkoani Singida wamemtaka mdogo wake Nyalandu, anayefahamika kwa jina la Peter Nyalandu kufika kituoni mara moja kwa ajili ya mahojiano ambayo hayajabainishwa.

error: Content is protected !!