Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nyalandu: Nikiwa Rais Tanzania, hakuna atakayeisoma namba
Habari za Siasa

Nyalandu: Nikiwa Rais Tanzania, hakuna atakayeisoma namba

Lazaro Nyalandu
Spread the love

LAZARO Nyalandu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati na mtia nia wa Urais kupitia chama hicho amesema, akiwa Rais wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaisoma namba. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Nyalandu ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 19 Julai 2020 wakati akirejesha fomu ya kukiomba chama hicho kimpitishe kuwa mgombea urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Tungependa mtu mwingine aingie katika kuiongoza nchi na CCM wasipate fursa ya kuisoma namba,” amesema Nyalandu, waziri wa zamani wa maliasili na utalii.

“Kuna ule mziki wanaoimba acha waisome namba lakini tutakaposhika dola na Mungu akijalia Nyalandu nikawa Rais hakuna Mwana-CCM, Mwana-Chadema wala Mtanzania yoyote ambaye sisi tutapenda aisome namba,” amesema.

Nyalandu amesema akiwa Rais kupitia Chadema ataimarisha fursa ya kila Mtanzania kupata haki anayostahili kupata pamoja na kuondoa sheria zote kandamizi ambazo zimewakwaza wananchi hasa suala la kunyimwa dhamana kwa mwenye kosa ambalo kisheria anastahili kupata dhamana.

“Tutafuta kutokupewa dhamana kwa Mtanzania yoyote kwa makosa ambayo kisheria anafaa kupewa dhamana, tutaanzisha mchakato wa katiba mpya mara moja na hadidu zetu za rejea zitaanzia kwenye katiba ya Mzee Warioba.”

Soma zaidi…

“Kama wewe ni mwana CCM usiichukulie Chadema poa, nenda kajipange kwenye Kata yako, Jimbo lako na Urais pia kwasababu tunakuja na tutakushinda, habari ya kuambiwa mtatangazwa mnadanganywa,” amesema.

Amesema Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kusema kuhusu uwazi na ukweli hivyo wenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wawe wawazi na wakweli kwa kumtangaza yoyote atakayeibuka mshindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!