July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyalandu: Matumizi mabaya ardhi ni tishio

Hifadhi ya Arusha

Spread the love

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora  yamekua tishio kwa  maeneo uhifadhi. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea)

Aidha, imepelekea  uvamizi wa maeneo hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo kinyume cha utaratibu. 

Nyalandu amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa kati ya Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) uliofanyika jijini hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu  utakaorithiwa na vizazi vijavyo  mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa.

 Amesema ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi hivyo amewataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji  kwa kuwekeza nje ya hifadhi.

 “Mtu anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu vizuri  lazima tutawanye  uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi” Amesema  Nyalandu

 Amesema  kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya nyingine  17 ziko katika hatua mbalimbali za uanzishwaji.

Hivyo amezitaka jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi katika kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanyamapori ya mwaka 1998.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard  Chambulo amesema  kuwa ili uhifadhi uweze kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na hati miliki za maliasili ili waweze kuzitunza vyema.

 Chambulo amesema  kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni nguzo muhimu sana kwa uhifadhi  itakayosaidia kuwa na utalii endelevu kwa vizazi vijavyo.

error: Content is protected !!