May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyalandu, Mathew wajiunga CCM, Rais Samia asema…

Lazaro Nyalandu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kanda ya kati akihutubia mkutano mkuu wa CCM mara baada ya kurejea kwenye chama hiko.

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepata pigo baada ya kuondokewa na wenyeviti wawili wa kanda na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Wenyeviti hao ni, Lazaro Nyalandu wa Kanda ya Kati na Suleiman Mathew wa Kanda ya Kusini.

Vigogo hao ambao kwa nafasi zao, walikuwa wajumbe wa kamati kuu, wametangaza uamuzi huo leo Ijumaa, tarehe 30 Aprili 2021, mbele ya Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.

Nyalandu aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii, alitangaza kuihama CCM, tarehe 30 Oktoba 2017 na kujiunga na Chadema.

Amedumu Chadema kwa siku 1,278 sawa na miaka mitatu na nusu ambapo amesme, “ukiwa ugenini, unaulizwa nyumbani unarudi lini. Nilikuwa naulizwa swali hili.”

“Watanzania, wameiona nyota yako (Rais Samia), wameguswa na kujawa na furaha kwa kuinuliwa nawe kwa kuwa Mungu alikuandaa na mkono hodari wa Mungu ukakuongoze katika kluwaongoza Watanzania wote.”

“Mama tuma neon lako likaponye kwa wale walioumia, mama na Rais wetu ukaitwe heri na shujaa kwa mioyo ya Watanzania na ukaongeze tabasamu juu ya nyuso zao,” amesema Nyalandu, aliyewahi kuwa mbunge wa Singida Mashariki

Kwa upande wake, Mathew amesema, ameamua kurejea nyumbani kuendelea kuwatumikia Watanzania chini ya Rais Samia.

Suleiman Mathew akiongea kwenye mkutano mkuu wa Ccm mara bade ya kujiunga kwenye chama hijo akitokea Chadema

Mara baada ya kumaliza kuzungumza, alisema “nawashukuru sana ndugu yetu Nyalandu kwa kurudi nyumbani, kule kwetu Zanzibar wana msemo, nyumba uliyoizoea kuihama ni kazi kweli kweli na wanaume wanaijua hilo.”

error: Content is protected !!