January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyalandu awageuka Wamarekani

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MB) akipokewa askari wa wanyamapori alipotembelea mbuga ya Ngorongoro

Spread the love

WAZIRI wa Maliasili na Utali, Lazaro Nyalandu amekipiga marufuku kikundi cha wanajeshi wastaafu wa Marekani (Vetpaw), kuingia katika mbuga za wanyama kikijifanya kupambana na majangili nchini kwa kutumia silaha za moto. Anaandika Charles Mseti, Mwanza (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani, Nyalandu amesema kuwa kikundi hicho kimekuwa kikitumia mitandao kujitangaza kuwa kinapambana na majangili kwa kuwapiga risasi za vichwa kinyume na sheria.

“Naagiza wakurugenzi wa Mamlaka ya Ngorongoro, Tanapa na Mkurugenzi wa Idara ya wanyamapori, kuhakikisha Wamarekani hao wanaondoka katika hifadhi mara moja,” amesema Nyalandu.

Amesema hakuna askari kutoka nje ya nchi anayeruhusiwa kuingia katika hifadhi akiwa na silaha, kwani jukumu la kupambana na majangili nchini, linafanywa na askari wa wanyamapori.

“Unajua kikundi hiki ni cha kizushi kimeingia nchini na kujitamba kwenye mitandao kwamba kinafanya kazi ya kupambana na ujangili Tanzania. Wanachafua jina la nchi na kuchangisha fedha duniani kwa kudanganya kuwa wanapambana na majangili,”amesema.

Nyalandu anaongeza kuwa, “kuanzia sasa naagiza Mamlaka ya ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA) kama ilifanya makubaliano yoyote na kikosi hicho ifute mara moja hayo makubaliano, waliofanya ama kama walikuwa na nia ya kufanya na matapeli hao watambue hao ni matapeli.”

error: Content is protected !!